Jumuiya
Pashavo inakua kwa maswali yenu. Uliza unachotaka kujua kuhusu AI, na shiriki prompti inayokusaidia.
Unataka kujua nini?
Tunasoma kila swali. Swali zuri linajibiwa kwa makala hapa Pashavo, ili kila mtu anufaike na jibu.
Tuandikie
Una swali, pendekezo, au umeona kosa? Tuandikie barua pepe.
nijuze@pashavo.comMaswali tuliyojibu
Majibu ya kwanza yanaandaliwa. Uliza swali lako sasa, linaweza kuwa la kwanza.
Prompti za jamii
Prompti zilizoshirikiwa na wasomaji. Tunazisoma kabla hazijaonekana hapa.
-
Nitengenezee maelezo mafupi ya WhatsApp Status kwa bidhaa hii: [bidhaa, bei, mji]. Mistari mitatu, Kiswahili cha kawaida, bila kutia chumvi.
Kutoka kwa Pashavo
-
Fupisha maandishi haya kwa aya mbili za Kiswahili rahisi, kisha orodhesha mambo matatu muhimu: [bandika maandishi]
Kutoka kwa Pashavo
-
Andika barua ya kuomba kazi ya [kazi] kwa [kampuni]. Mistari 12, Kiswahili cha kiofisi, taja uzoefu huu: [uzoefu wako].
Kutoka kwa Pashavo
-
Eleza [dhana ngumu] kama unamwambia mtu asiyesoma chuo. Tumia mfano wa maisha ya Tanzania. Usizidi maneno 150.
Kutoka kwa Pashavo
-
Nimenunua bidhaa kwa [bei ya kununua]. Nataka faida ya asilimia [idadi]. Nionyeshe hesabu hatua kwa hatua na bei ya kuuza.
Kutoka kwa Pashavo
-
Tafsiri aya hii kwa Kiswahili cha kawaida kinachosikika Dar, si Kiswahili sanifu cha vitabu: [bandika aya]
Kutoka kwa Pashavo
-
Nipangie wiki yangu. Hizi ndizo kazi zangu: [orodha]. Weka kazi ngumu asubuhi, na uniachie nafasi ya dharura kila siku.
Kutoka kwa Pashavo
-
Wewe ni mwalimu wa [somo] wa [kidato]. Nitengenezee maswali 10 ya mazoezi kuhusu [mada], kwa Kiswahili rahisi, na uweke majibu mwishoni.
Kutoka kwa Pashavo
Shiriki prompti yako
Una prompti inayokusaidia shuleni, kazini au biasharani? Ituandikie. Tutaisoma kabla ya kuichapisha.
Jinsi jumuiya inavyofanya kazi
Tunasoma kila kitu
Kila swali na kila prompti vinasomwa kabla ya kuonekana kwenye tovuti. Hakuna kinachochapishwa moja kwa moja.
Faragha yako
Jina na mji si lazima, na hatuuzi taarifa zako kwa mtu yeyote.
Heshima kwanza
Hatuchapishi matusi, siasa za vyama, utapeli wala matangazo.